Mafunzo endelevu ya Walimu kazini (MEWAKA)
Je una akaunti kwenye mfumo?
Ingia kwa kutumia namba ya simu
Je ni mara yako kwanza kwenye mfumo?
Fungua akaunti mpyaKwa watumiaji wenye simu janja
Nenda Google Play au Apple Store na utafute Moodle, kisha uipakue na uisakinishe kwenye kifaa chako cha mkononi. Kwenye URL, ingiza https://tcpd.tie.go.tz
Moduli za MEWAKA
- Moduli Zilizopo
- Moduli za Masomo
- Moduli za Mbinu za Kufundishia
- Kufundisha Madarasa Makubwa
- Kufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum
- Usimamizi wa Darasa
- Matumizi ya TEHAMA
- Ngazi za Moduli
- Mbinu za Kujifunza
Mfumo huu una aina mbalimbali za moduli zinazolenga kuimarisha ujuzi wa walimu. Kuna moduli zinazohusu masomo kwa mano Hesabu na Giografia, pamoja na moduli ambazo hufundisha mbinu za kufundishia bila kujali aina ya somo husika.
Jiongeze ujuzi katika masomo mbalimbali kama vile Kiingereza, Kemia, Baiolojia, Hisabati, Historia, na mengineyo. Kila moduli ya somo imeandaliwa kwa ustadi kutoa maarifa ya kina na mbinu za kufundishia zilizothibitishwa na wataalamu wa masomo hayo.
Gundua mbinu mpya za kufundishia kupitia moduli zetu za mbinu za kufundishia. Mada kuu kwenye moduli hizi ni pamoja na:
Jifunze mbinu bora za kusimamia na kuvutia makundi makubwa ya wanafunzi.
Jifunze jinsi ya kuunda mazingira ya darasa yanayojumuisha na kuheshimu mahitaji mbali mbali ya wanafunzi wataki wa kujifunza.
Pata maarifa kuhusu jinsi ya kudumisha mazingira chanya na yenye tija darasani.
Elewa jinsi ya kujumuisha teknolojia kwa ufanisi katika mbinu zako za kufundishia.
Maudhui yetu yameandaliwa kwa umakini ili kutosheleza mahitaji ya walimu katika ngazi mbalimbali za elimu. Mfumo una moduli kwa ajili ya walimu wa Shule za awali, shule za msingi, shule za sekondari na pia vyuo vya ualimu.
Jukwaa lina aina kuu mbili za moduli, moduli za kujifunza binafsi ambapo mwalimu anatarajiwa kujifunza kozi peke yake na kwa kasi yake mwenyewe, na moduli za jumuiya ya kujifunza ambapo moduli inapaswa kufanywa na kikundi cha walimu katika shule. Katika Jumuiya za Kujifunza (JzK), msimamizi wa rika anachukua nafasi kuu.