Moduli za MEWAKA

  1. Moduli Zilizopo
  2. Mfumo huu una aina mbalimbali za moduli zinazolenga kuimarisha ujuzi wa walimu. Kuna moduli zinazohusu masomo kwa mano Hesabu na Giografia, pamoja na moduli ambazo hufundisha mbinu za kufundishia bila kujali aina ya somo husika.

  3. Moduli za Masomo
  4. Jiongeze ujuzi katika masomo mbalimbali kama vile Kiingereza, Kemia, Baiolojia, Hisabati, Historia, na mengineyo. Kila moduli ya somo imeandaliwa kwa ustadi kutoa maarifa ya kina na mbinu za kufundishia zilizothibitishwa na wataalamu wa masomo hayo.

  5. Moduli za Mbinu za Kufundishia
  6. Gundua mbinu mpya za kufundishia kupitia moduli zetu za mbinu za kufundishia. Mada kuu kwenye moduli hizi ni pamoja na:

  7. Kufundisha Madarasa Makubwa
  8. Jifunze mbinu bora za kusimamia na kuvutia makundi makubwa ya wanafunzi.

  9. Kufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum
  10. Jifunze jinsi ya kuunda mazingira ya darasa yanayojumuisha na kuheshimu mahitaji mbali mbali ya wanafunzi wataki wa kujifunza.

  11. Usimamizi wa Darasa
  12. Pata maarifa kuhusu jinsi ya kudumisha mazingira chanya na yenye tija darasani.

  13. Matumizi ya TEHAMA
  14. Elewa jinsi ya kujumuisha teknolojia kwa ufanisi katika mbinu zako za kufundishia.

  15. Ngazi za Moduli
  16. Maudhui yetu yameandaliwa kwa umakini ili kutosheleza mahitaji ya walimu katika ngazi mbalimbali za elimu. Mfumo una moduli kwa ajili ya walimu wa Shule za awali, shule za msingi, shule za sekondari na pia vyuo vya ualimu.

  17. Mbinu za Kujifunza
  18. Jukwaa lina aina kuu mbili za moduli, moduli za kujifunza binafsi ambapo mwalimu anatarajiwa kujifunza kozi peke yake na kwa kasi yake mwenyewe, na moduli za jumuiya ya kujifunza ambapo moduli inapaswa kufanywa na kikundi cha walimu katika shule. Katika Jumuiya za Kujifunza (JzK), msimamizi wa rika anachukua nafasi kuu.

Wasiliana nasi kupita anwani hii:

Name:

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),

S.L.P:

35094, 4112 Dar es Salaam,

Mahali:

Eneo la Mikocheni, 132 Barabara ya Ali Hassan Mwinyi,

Simu:

+255-735-041168

Simu:

+255-735-041168

Tovuti:

https://www.tie.go.tz